Connect with us

Makala

Yanga sc Kuivaa Namungo Fc

Klabu ya Yanga sc itacheza mchezo wake wa ligi kuu nchini dhidi ya Namungo Fc siku ya Jumamosi April 23 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili wa ligi kuu nchini inayodhaminiwa na benki ya biashara ya Nbc.

Katika mchezo wa awali uliofanyika katika uwanja wa Ilulu mkoani Lindi Yanga sc iliponea chupuchupu kupoteza mchezo huo ikifanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika za mwishoni kwa penati baada ya Feisal Salum kuangushwa ndani ya eneo la 18 huku Penati hiyo ikilalamikiwa na wadau wa soka nchini ambapo ilisababisha mwamuzi wa mchezo huo kufungiwa na bodi ya ligi.

Awali kwa mujibu wa ratiba ya ligi kuu klabu ya Yanga sc baada ya kucheza na Azam Fc kisha Geita Gold Fc katika mchezo wa hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la shirikisho ilipaswa kusubiri mpaka tarehe 30 mwezi huu ambapo ingecheza na Simba sc mchezo wa ligi kuu unaosubiriwa na wadau wengi.

Tayari bodi ya ligi kuu nchini imetangaza mabadiliko hayo ya tarehe za michezo huku ikiwekwa wazi kwamba hapo awali michezo hiyo haikupangiwa ratiba kutokana na ushiriki wa vilabu vya Yanga sc,Simba sc,Azam Fc na Biashara katika michuano ya kimataifa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala