Home Makala Wanne Kuwania Saini Ya Nyota Huyu

Wanne Kuwania Saini Ya Nyota Huyu

by Sports Leo
0 comments

Miamba ya soka ndani ya Ligi Kuu England ikiwa ni pamoja na Liverpool, Manchester United na Arsenal imegongana kwenye kuwania saini ya winga anayekipiga ndani ya klabu ya Monaco, Wissam Ben Yedder.

Nyota huyo mwenye miaka 29 alijiunga na AS Monaco akitokea klabu ya Sevilla na amekuwa  nyota ndani ya Ligue msimu huu ambapo ametupia mabao 18 akiwa amecheza mechi 26 hii imemfanya kuwavutia klabu nyingi kubwa ambazo zinahitaji kuipata saini yake kwa ajili ya kumtumia msimu ujao wa 2020/21.

Mbali na timu ambazo zinashiriki Ligi Kuu England,pia timu zinazoshiriki La Liga zinahaha kuipata saini ya nyota huyo huku Real Madrid ikitajwa kuwa mstari wa mbele.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited