Connect with us

Makala

Waarabu Waifuata Yanga sc Dar

Timu ya soka ya Al Hilal Tayari imeanza safari ya kuja nchini kuja kuvaana na Yanga sc mchezo wa kwanza katika hatua ya pili ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika mchezo utakaofanyika siku ya Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo ambao Yanga sc atakua mwenyeji unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kutokana na kiu ya Yanga sc kufuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika huku mara ya mwisho kufuzu ikiwa ni mwaka 1998 ambapo baada ya hapo wamekua wakiangukia katika kombe la shirikisho pekee ambapo wamefika makundi mara mbili kwa miaka ya hivi karibuni.

Al Hilal imeanza safari ya kuja jijini Dar es salaam ikitokea Congo ambako iliweka kambi ya muda mfupi ya maandalizi na kufanikiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Tp Mazembe na sasa hivi leo wapo njiani kuja nchini ambapo wanatarijiwa kutua jioni hii ya leo tayari kwa mechi hiyo ya keshi kutwa Jumamosi.

Baada ya mchezo huo itakua ni kazi kwa Yanga sc kusafiri mpaka jijini Khartoum Sudan kuvaaana na waarabu hao ambao wanasifika kuwa na mashabiki wakorofi hasa kwa kushangilia na staili ya kuwasha moto na kupiga ngoma mwanzo mpaka mwisho wa mchezo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala