Connect with us

Makala

Wa Kawaida Kabisa

Afisa habari wa klabu ya Yanga sc Ally Kamwe amesema kuwa klabu hiyo haiwahofii wapinzania wao katika raundi ya pili ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika ambao ni klabu ya Al Hilal Fc ya nchini Sudan licha ya kuwa wapinzani hao wana kikosi cha gharama zaidi.

Kamwe alisema hayo wakati akifanya mahojiano na kituo cha habari cha Wasafi Fm ambapo alisisitiza kuwa Yanga sc wana kikosi bora na chenye muungano kushinda Wasudan hao kwa maana wanategemea zaidi uwezo wa mchezaji mmoja mmoja.

“Yanga ni Timu bora Tanzania, kwa Squad ambayo tuko nayo, Squad ambayo imekwenda unbeaten michezo 41 ya Ligi,Hii rekodi angekuwa nayo Al Hilal, Yanga tusingelala, lakini watu hawawaambii Al Hilal kama wanakuja kucheza na Dubwasha ambalo limecheza michezo 41 bila kufungwa, na hiyo michezo 41 wapambe wenu wapo,”Alisema Kamwe

Mbali na mchezo huo pia aligusia namna klabu hiyo ilivyofanya mchakato wa mabadiliko halisi kuelekea katika mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu hapa nchini “Nilikuwa nasikia tu kuhusu mabadiliko lakini nimekuja kuyaona Yanga, hakuna Timu ikiyofanya Mabadiliko Sahihi ya Mpira kuliko Yanga Sc, Injinia amelipa Pesa nyingi sana La liga kupata huo ushauri wa kiendeshaji”

Yanga sc itacheza na Al Hilal ya kocha Florent Ibenge katika mchezo wa kwanza ambao utafanyika hapa nchini siku ya Jumamosi Oktoba 8 na marudiano yatafanyika nchini Sudan siku ya Oktoba 16.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala