Connect with us

Makala

Tuzo Ya Mchezaji Bora 2020 Yafutwa

Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) limetangaza kufuta tuzo za soka zinazotolewa na Shirikisho hilo mwaka huu kutokana na janga la virusi vya Corona ambazo zilitarajiwa kutolewa jijini Milan nchini Italia, Septemba 2020.

Washindani wawili duniani ambao ni Lionel Messi anayekipiga Barcelona na Cristiano Ronaldo wa Juventus  hawatakuwa na cha kubeba mwaka huu Kwenye kipengele cha mchezaji bora wa mwaka.

Gianni Infantino, ambaye ni Rais wa FIFA amekuwa akiweka wazi msimamo wake kuwa wanachukua tahadhari kubwa dhidi ya janga la virusi vya Corona na kuhusu tuzo za Ballon d’Or ambazo zimekuwa zikitolewa kila mwaka tangu 1956 haijulikani hatma yake mpaka sasa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala