Connect with us

Makala

TFF Yaunda Kamati Ya Ushindi Taifa Stars

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia, ameunda kamati ya ushindi ya timu ya Taifa (Taifa Stars) ambayo mwenyekiti wake ni Ghalib Said Mohammed (GSM) huku makamu mwenyekiti akiwa ni Salim Abdallah na Katibu wake ni Mhandisi Hersi Said.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF mapema leo, wajumbe wa Kamati hiyo watakuwa Haji Manara, Patrick Kahemele, Jerry Muro Pamoja na Abdallah Bin Kleb.

Kamati hiyo itasaidia kuipa motisha timu ya Taifa ya Tanzania kuweza kushinda katika michuano yake ya kirafiki na timu nyingine za kitaifa.

Taifa Stars ilipokea Kichapo katika mchezo wa kirafiki juzi,Octoba 11, ambapo Burundi ilijipatia ushindi wa bao 1-0 ikiwa ugenini.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala