Home Makala Tariq Arejea Yanga

Tariq Arejea Yanga

by Sports Leo
0 comments

Kikosi cha Yanga leo kinaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar.

Mchezo huo utapigwa keshokutwa Jumatano kwenye uwanja wa Taifa (kama hakutakuwa na mabadiliko).

Kuelekea mchezo huo, habari njema kwa Yanga ni kurejea kikosini kwa mshambuliaji wake Tariq Seif Kiakala ambaye alikuwa akisumbuliwa na majeraha ya nyama za paja.

Tariq aliukosa mchezo dhidi ya Simba pamoja na michuano ya kombe la Mapinduzi kutokana na tatizo hilo.

Daktari wa Yanga Sheck Mngazija amethibitisha kuwa nyota huyo yuko fiti na ataungana na timu kwenye mazoezi ya leo.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited