Sven Akiandaa Kikosi Kwa Biashara

0

Kocha mkuu wa Simba SC,Sven Vandenbroeck amesema kwa sasa anakiandaa kikosi chake maalum kwa mchezo ujao wa ligi kuu bara utakaofanyika uwanja wa Mkapa dhidi ya Biashara United siku ya Jumapili.

Sven ameyasema hayo baada ya kutoa sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar katika mchezo wa jana uliofanyika katika uwanja wa Jamuhuri mkoani Morogoro.

Mchezo wa jumapili utakuwa mchezo wa kwanza kwa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu bara kucheza katika uwanja wa nyumbani baada ya mbili zilizoisha kucheza ugenini.

Wachezaji na benchi la ufundi wamepokea changamoto katika mchezo uliyopita na wamezipokea ili kujipanga kwa mchezo ujao na kuweka mbinu mpya watakazozitumia dhidi ya Biashara United.

Leave A Reply

Your email address will not be published.