Connect with us

Makala

Suprise Kibao Singida Big Stars

Timu ya soka ya Singida Big Stars imefanya tamasha la kufungua msimu mpya la Singida Big day lililofanyika katika uwanja wa Liti mkoani humo ambapo mastaa kibao walitambulishwa.

Licha ya msanii Harmonize kutumbuiza katika tamasha hilo pia mashabiki wa soka mkoani humo walipata furaha zaidi kutokana na kufahamu kuwa kocha Hans Van De Pluijm kuwa ndie kocha mkuu wa klabu hiyo akisaidiwa na Nizar Khalfan na Mathias Lule huku pia Meddie Kagere na Paschal Wawa wakitambulishwa kuwa wachezaji wapya wa timu hiyo.

Suprise nyingine ni uwepo wa mastaa watatu kutoka nchini Brazil ambao nao wanaonekana wana viwango vizuri kiasi cha kucheza mpira mkubwa wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya Zanaco Fc iliyomalizika kwa wenyeji kushinda bao moja kwa bila likifungwa na Deus Kaseke.

Singida Big Stars imepanda daraja kucheza ligi kuu msimu huu ambapo mpaka sasa imesajili mastaa waliotamba katika ligi kuu nchini akiwemo Amis Tambwe,Said Ndemla,Juma Abdul,Yassin Mustapha,Paulo Godfrey na wengineo wengi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala