Stars Tayari Kuivaa Tunisia Kesho

0

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)Etienne Ndayiragije amesema kuwa amekiandaa kikosi chake vizuri kwa ajili ya mchezo wa kufuzu Afcon kesho Novemba 13 ,dhidi ya Tunisia na tayari kikosi kimeshawasili nchini humo ikiwa ni kwa ajili ya maandaizi ya mwisho ya mchezo huo wa kesho.

Mchezo huo utachezwa uwanja wa Olympique De Rades nchini Tunisia bila ya uwepo wa mashabiki kutokana na Shirikisho la soka Afrika (Caf) kutaka iwe hivyo ili kuchukua tahadhari dhidi ya Corona na ule wa marudio utachezwa Novemba 17 uwanja wa Mkapa huku nusu ya mashabiki wakiruhusiwa kutazama mchuano huo na Caf wenyewe.

Stars katika michuano ya Afcon ipo kundi J ina pointi tatu ikiwa inakutana na Tunisia ambao ni vinara wakiwa na pointi sita hivyo ikishinda itaongeza nafasi ya kunusa hatua ya kufuzu Afcon 2021 nchini Cameroon.

Leave A Reply

Your email address will not be published.