Connect with us

Makala

Singida Big Stars Yaiwahi Simba sc

Klabu ya Singida Big Stars tayari imewasili mapema jijini Dar es salaam kwa ajili ya mchezo wake wa ligi kuu dhidi ya Simba sc utakaofanyika siku ya Februari 3 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Awali timu hizo ziligawana alama katika sare ya 1-1 katika uwanja wa Liti mjini Singida ambapo mabao ya mchezo huo yalifungwa na Deus Kaseke na Peter Banda ambapo pia Singida Big Stars walifanikiwa kuonyesha mchezo mzuri kwa dakika kadhaa wakipishana na Simba sc.

Katika mchezo Singida itawakosa Deus Kaseke ambae amefungiwa na bodi ya ligi michezo mitatu kwa kujihusisha na imani za kishirikina katika mchezo dhidi ya Azam Fc huku pia Simba sc ikifurahia urejeo wa Peter Banda na Henock Inonga ambao tayari wameanza mazoezi toka wiki iliyopita.

Ugumu wa mchezo huo unatokana na pengo la alama baina ya timu hizo ambapo Simba sc ina alama 50 huku Singida Big Stars ikiwa na alama 43 ambapo kila timu ina lengo la kuhakikisha ubingwa unapatikana mwishoni mwa msimu huu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala