Simba wamerudi tena jijini Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba katika mechi yake dhidi ya Alliance wakisimamiwa na kocha wao mkuu Sven Vanderbroeck raia wa Ubelgiji.
Alliance iliyochini ya Felix Minziro ina kisasi kizito na Simba baada ya kupoteza michezo miwili mmoja akiwa amechapwa na Simba mabao 2-0 katika uwanja wa nyumbani CCM Kirumba na mara ya pili uwanja wa taifa walifungwa mabao 5-1 hivyo ina mizigo ya kufungwa jumla ya mabao 7-1 na Simba 2018/19.
Hesabu za Simba ni kuchukua pointi sita za kanda ya ziwa ikiwa tatu walishachukua juzi baada ya kuwafunga Mbao Fc 2-1 hivyo tatu zilizo baki ni za leo kutoka kwa Alliance Fc.