Connect with us

Makala

Simba sc Yazindua Simba day 2022

Klabu ya soka ya Simba sc imefanikiwa kufanya uzinduzi wa Tamasha la siku ya Simba day ambapo wamezindua rasmi shamrashamra kuelekea siku hiyo (Simba week 2022) ambapo kutakua na shughuli mbalimbali za kijamii zitafanyika katika wiki hiyo.

Uzinduzi huo ulifanyika Jumapili Julai 31 katika viwanja vya Mbagala zakhiem na kuhudhuriwa na Afisa Mtendaji mkuu wa klabu hiyo Babrah Gonzalez aliyeambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Murtaza Mangungu,Asha Baraka,Hassan Dalali na wengineo huku msanii Zuchu akitumbuiza sherehe hizo.

Simba week ni wiki maalimu kuelekea Siku ya Simba day ambayo hufanyika kila mwaka siku ya August 8 ambayo ni siku ya mapumziko kwa wafanyakazi nchini huku tayari tiketi kwa ajili ya tamasha hilo zikiwa tayari zimeanza kuuzwa ambapo bei ya juu ni laki mbili na ya chini ni shilingi elfu 5.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala