Connect with us

Makala

Simba sc Yawatema Kagere,Mugalu

Klabu ya Simba sc imewatema mastaa wake watatu wakiwemo  washambuliaji Meddie Kagere na Chris Mugalu pamoja na kiungo Thaddeo Lwanga baada ya kukubaliana kuvunja mikataba ya mwaka mmoja iliyobaki.

Wachezaji hao walijiunga na kambi ya mazoezi ya klabu hiyo nchini Misri lakini walirejea mapema kabla ya wengine kuja kufanya makubaliano ya kuvunja mikataba baada ya kocha Zoran Maki kutoridhishwa na viwango vyao ambapo awali aliomba muda ili awaangalie vizuri.

Mugalu na Kagere hawakuwa na msimu mzuri uliopita baada ya kushindwa kufurukuta na kuifanya Simba sc imalize ligi bila taji lolote la maana baada ya kunyakua mataji mfululizo kwa kipindi cha miaka minne.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala