Connect with us

Makala

Simba Sc Yatuma Ofa kwa Mwamnyeto

Klabu ya Simba Sc imetuma ofa ya kumsajili beki Bakari Nondo Mwamnyeto kwa menejimenti ya mchezaji huyo baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Yanga sc ambayo nayo imeonyesha nia ya kuendelea nae.

Mwamnyeto ambaye mkataba wake unamalizika juni 30 mwaka huu yuko huru kuzungumza na klabu yeyote huku Yanga sc ikiwa imeshaanza mazungumzo ya kumuongezea mkataba ambayo yamefikia mahali pazuri.

Carlos Mastermind ambaye anamsimamia mchezaji huyo amesema kuwa mpaka sasa bado hawajafanya maamuzi kuwa wapi atasaini kwa maana ya wanedelea na mazungumzo na Yanga sc huku akiwa amepokea tayari ofa za klabu zingine ikiwemo ya Simba sc ambayo ni ofa nzuri pia.

“Soka ni kazi ya mchezaji ndio maana tumepata muda wa kuzichambua tuone ni ipi itamfaa. Kama unavyojua usajili ulivyo lolote linaweza likatokea,” Carlos Sylivester, meneja wa wa nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto akimzungumzia mchezaji huyo aliyemaliza mkataba katika timu hiyo.

Mwamnyeto amekua na misimu mizuri akiwa Yanga sc tangu ajiunge nao msimu wa 2020 ambapo alichaguliwa kuwa nahodha wa klabu hiyo mpaka sasa akiwa na mafanikio makubwa ikiwemo kutwaa mataji ya ligi kuu na kombe la Shirikisho kwa mara ya tatu mfululizo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala