Connect with us

Makala

Simba sc Yasajili Kimya Kimya

Ni mwendo wa kimya kimya ndio ambao viongozi wa klabu ya Simba sc wameuchagua baada ya kufanya sajili takribani tano lakini mpaka sasa wahajazitangaza kokote Sportleo imebaini.

Tayari klabu hiyo kupitia kwa mwenyekiti wa bodi Salim Abdalah ”Try Again”imemalizana kwa kuwapa mikataba Moses Phiri ambaye tayari imemtambulisha kwa mashabiki wa klabu hiyo kama usajili wa kwanza huku pia ikiwa imewasainisha mikataba Habib Kyombo ambaye awali alisaini Singida Big Stars lakini Simba sc ikatumia ukubwa wake kubadili mawazo ya mchezaji na kumfanya akanunue mkataba wake kule Singida Big Stars.

Pia kiraka Nassoro Kapama nae tayari amesaini klabuni hapo akiwa kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake Kagera Sugar na tayari klabu yake ya zamani imeshamtakia kila la kheri katika malisho yake mapya huku Msimbazi japo klabu haijatangaza ikiwa imefanya kimya kimya kama ilivyo sera yao ya usajili ya sasa.

Kwa upande ya sajili za kimataifa mbali na Phiri pia klabu hiyo imewasajili viungo washambuliaji Augustine Okrah na Nelson Okwa kutoka Afrika Magharibi pamoja na mshambuliaji wa Vipers Fc Cesar Manzoki ambaye alitua kimya kimya kusaini na kuondoka kimya kimya.

Sambamba na kusajili kimya kimya pia klabu hiyo imewaacha Meddie Kagere,Pascal Wawa,Yussuph Mhilu(Mkopo) huku pia panga likiendelea kwa mastaa wengine ili kuhakikisha usajili unakwenda sawa ili kushindana katika ngazi ya kimataifa ambapo awali waliishia robo fainali.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala