Home Makala Simba sc Yapigwa Mbeya

Simba sc Yapigwa Mbeya

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc imeshindwa kuibuka na ushindi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City katika mchezo uliofanyika katika uwanja kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Simba sc iliingia katika mchezo ikiwa na matumaini ya kuibuka na ushindi huku ikiwaanzisha mabeki Josh Onyango na Henock Inonga waliosaidiwa na Shomari Kapombe,Aishi Manula na Mohamed Hussein ukuta ambao uliaminika kuwa imara lakini kutojipanga vizuri kwa walinzi hao kulisababisha wenyejin kupata bao la kuongoza kupitia kwa Paul Nonga dakika ya 19 bao ambalo lilidumu mpaka kipindi cha mapumziko.

Awali kipindi cha pili Simba sc walifanya mabadiliko wakimtoa Mzamiru Yassin na kumuingia John Bocco huku wakishindwa kuzitendea haki nafasi kadhaa za kufunga walizotengeneza huku wakifanikiwa kupata penati baada ya mlinzi wa Mbeya city kuunawa mpira ndani ya box ambapo mpigaji Chris Mugalu alikosa penati hiyo baada ya kugonga mwamba na kutua mikononi mwa kipa Deogratius Munishi.

banner

Simba sc walifanya mabadiliko kwa kumuingiza Pape Osmane Sakho na Meddie Kagere lakini uimara wa mabeki wa Mbeya City hasa Kipa Deogratius Munishi uliwafanya Simba sc kutoka uwanjani wakiwa wamekosa alama tatu za mchezo huo na kufanya tofauti ya alama kufika nane dhidi ya mpinzani wake Yanga sc anayeongoza ligi akiwa na alama 32.

kufuatia ushindi huo wa jana Mbeya city imepanda mpaka nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na alama 19 ikiwa imecheza michezo 12.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited