Connect with us

Makala

Simba sc Yamtambulisha Kocha wa Vipers Fc

Klabu ya Simba sc imemsainisha mkataba wa miaka miwili kocha Roberto Oliveira aliyekua akiifundisha Vipers Fc ya nchini Uganda kujiunga na klabu hiyo kuelekea duru la pili la ligi kuu pamoja na hatua ya makundi ya michuano ya kimataifa ya kombe la klabu bingwa barani Afrika.

Oliveira raia wa Brazil aliyedumu Vipers Fc kwa misimu takribani miwili akiwapa mataji ya kombe la Uganda  na ligi kuu ya nchini humo katika miezi kumi na nne aliyokaa klabuni hapo huku akifanikiwa kuipeleka Vipers Fc katika hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika ambapo wamepangwa kundi moja na Simba sc ambapo katika kundi hilo C pia lina klabu za Raja Casablanca na Horoya Fc.

Kutokana na kusajiliwa kwa kocha huyo sasa kocha Juma Mgunda atakua kocha msaidizi namba moja na Seleman Matola atakua kocha msaidizi namba mbili kwa mujibu wa Mwenyekiti wa klabu hiyo Murtaza Mangungu.

Kocha huyo mapema baada ya utambulisho alielekea Zanzibar kuungana na kikosi cha klabu hiyo ambacho kitakua na mchezo wa kombe la mapinduzi dhidi ya Mlandege Fc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala