Connect with us

Makala

Simba sc Yakwaa Kisiki

Klabu ya Simba sc imeshindwa kuibuka na alama tatu katika mchezo wa ligi kuu uliomalizika jioni hii katika uwanja wa Liti Mkoani Singida baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Singida Big Stars.

Ikianza na Moses Phiri,Pape Osmane Sakho,Mzamiru Yassin na Kibu Dennis katika eneo la mbele huku katikakati akicheza Jonas Mkude na Sadio Kanoute ilikua ngumu kwa Simba sc kufanya mashambulizi mara kwa mara katika kipindi cha kwanza baada ya Singida Big Stars kufanikiwa kumiliki kiungo ambapo uwepo wa Said Ndemla,Deus Kaseke na Bruno Gomes uliwazidi maarifa na kasi Simba sc.

Singida Big Stars walipata bao la mapema dakika ya 11 ya mchezo kupitia kwa Deus Kaseke aliyemalizia kazi ya Said Ndemla ambapo bao hilo lilidumu mpaka kipindi chote cha kwanza licha ya Simba sc kupata nafasi kadhaa za kufunga lakini walishindwa kuzitumia.

Kipindi cha pili Simba sc ilimuingiza Peter Banda kuchukua nafasi ya Jonas Mkude ambapo kasi ya kushambulia iliongezeka kupitia Banda,Phiri na Kibu huku Sakho akicheza kama kiungo namba 10 ambapo Simba sc ilipata bao la kusawazisha dakika ya 59 likifungwa na Peter Banda baada ya kipa wa Singida kuisindikiza krosi wavuni.

Licha ya Simba sc kupata bao hilo Singida Big Stars walicheza kwa kujihami muda mwingi wa mchezo huku wakishambulia kwa kushtukiza lakini kukosa umakini kwa wachezaji wa Simba sc eneo la mbele kulifanya mpaka dakika tisini zinamalizika mchezo uishe kwa sare.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala