Klabu ya Simba Sc imezidi kujisogeza kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini baada ya kuifunga timu ya Pamba Jiji Fc kwa mabao 5-1 katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini uliofanyika katika uwanja wa Kmc Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
Simba sc ilipata mabao hayo kupitia kwa Jean Charles Ahoua aliyefunga mabao matatu kipindi cha kwanza akianza na penati dakika ya 16 kisha alifunga kwa faulo dakika ya 37 na bao la kichwa akimalizia krosi ya Ellie Mpanzu dakika ya 48.
Pamba Jiji Fc walijitahidi kufurukuta lakini Simba sc iliwazidi ujanja katika maeneo mengi mchezoni ambapo pia Lionel Ateba alifunga mabao mawili dakika za 80 na 84 ambapo hasa bao lake la pili alilofungwa kwa shuti la ustadi mkubwa.
Pamba jiji Fc hawakutoka hivihivi ambapo Methew Momanyi alifunga bao la kufutia machozi kutokana na uzembe wa mabeki wa Simba sc ambapo aliuchopu vizuri mpira uliomshinda kipa Moussa Camara dakika ya 86 ya mchezo.
Simba sc sasa imefikisha alama 66 katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kuu ya Nbc huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi ambapo Yanga sc anaongoza msimamo wa ligi akiwa na alama 70.