Connect with us

Makala

Simba sc Yaifunga Asante Katoko

Klabu ya Simba sc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Asante Katoko ya nchini Ghana katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa nchini Sudan ambayo inafanyika kwa mwaliko maalumu wa klabu ya Al Hilal ya nchini humo.

Licha ya Simba sc kutanguliwa kufungwa,Agustin Okra dakika ya 19 ambaye aliweza kuweka usawa kwenye mchezo huo kwa kuwa Simba walianza kutunguliwa huku Pape Sakho alipachika bao moja dakika ya 26 na  mwamba wa Lusaka Clatous Chama alitupia mabao mawili  dakika ya 42 kwa mkwaju wa penalti na dakika ya 79.

Kiwango kibovu cha mabeki wa Simba sc kiliwapa Mabao mawili  Asante Kotoko yaliyopatikana kupitia kwa Mukala dakika ya 9 ambaye alikuwa wa kwanza kufunga  na Amankona yeye alifunga bao dakika ya 79.

Seleman Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa mashindano hayo yatawapa nguvu ya kufanya maandalizi mazuri kwenye mechi za ligi na za kimataifa.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala