Connect with us

Makala

Simba Sc Yafuzu Crdb Cup

Ushindi wa mabao 3-0 ilioupata klabu ya Simba Sc katika mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya Tma Stars umeifanya kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.

Simba sc imepata ushindi katika mchezo huo uliofanyika mapema jioni ya leo katika uwanja wa Kmc Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam mbele ya mashabiki kiasi waliojaa uwanjani hapo.

Kocha Fadlu Davis aliwapumzisha Ellie Mpanzu na Steven Mukwala huku golini akianza Ally Salim badala ya Moussa Camara ambaye ni majeruhi akiungana na Che Malone Fondoh ambaye naye anasumbuliwa na majeraha.

Simba sc ilipata bao la kwanza dakika ya 18 ya mchezo kupitia kwa Valentino Nouma aliyepiga faulo kali iliyojaa moja kwa moja golini huku pia dakika moja baadae Nouma alipiga krosi iliyookolewa vibaya na Sixtus Sabilo na kujaa wavuni.

Simba Sc ilipata bao la tatu dakika ya 75 likifungwa kwa kichwa na Lionel Ateba akiunganisha krosi ya Kelvin Kijiri na ndio bao lililohitimisha kalamu ya mabao kwa Simba sc.

Sasa Simba sc itasubiri droo ya michuano hiyo ili kujua itakutana na nani katika hatua ya 16 bora ili kupata washindi nane watakaoingia robo fainali ya michuano hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala