Klabu ya Simba Sc imefanikiwa kuchukua alama tatu katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini dhidi ya Klabu ya Jkt Tanzania uliofanyika Mei 5 2025 katika uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo jijini Dar es Salaam.
Â
Simba sc ambayo ilipata alama tatu kwa shida katika mchezo uliopita dhidi ya Mashujaa Fc ilikutana na upinzani mkali kutoka kwa vijana hao wa kocha Ahmed Ally kutokana na mbinu zake nzuri za kushambulia na kujilinda.
Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa matokeo ya suluhu lakini dakika 10 za kipindi cha pili zilitosha kuipatia bao Simba sc likifungwa na Fabrice Ngoma baada ya kazi nzuri ya Joshua Mutale aliyempasia Steven Mukwala na kutoa pasi kwa mfungaji.
Mpaka dakika tisini zinakamilika Simba Sc iliondoka na ushindi wa bao moja pekee na kuchukua alama tatu muhimu.
Simba sc sasa imefikisha alama 63 huku ikiwa na michezo 24 ya ligi kuu pungufu ya michezo miwili kutoka kwa Yanga sc ambao wanaongoza ligi mpaka sasa kwa alama 70.