Connect with us

Makala

Simba sc Vs Ihefu Fc Shirikisho

Klabu ya Simba sc itavaana na Ihefu Fc katika mchezo wa kombe la shirikisho nchini kwa mujibu wa droo iliyofanyika mapema hivi leo katika ofisi za wadhamini wa michuano hiyo za Azamtv jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa Droo hiyo iliyoongozwa na Said Maulid staa wa zamani wa Yanga sc na Bonifasi Pawasa staa wa zamani wa Simba sc imeonyesha kuwa Simba sc itaanzia nyumbani huku endapo moja kati ya klabu hizo zitafuzu basi zitavaana na mshindi kati ya Azam Fc na Mtibwa Sugar.

Mwaka jana katika michuano hii Simba sc iliishia katika hatua ya nusu fainali ambapo ilifungwa na Yanga sc bao 1-0 huku Yanga sc ikifanikiwa kuchukua kombe hilo baada ya kuifunga Coastal Union katika mchezo wa fainali jijini Arusha.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala