Home Makala Simba Sc Kujiuliza Kwa Jkt Tanzania

Simba Sc Kujiuliza Kwa Jkt Tanzania

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba Sc leo April 5 2025 inarudi tena uwanjani kuvaana na wenyeji wao maafande wa JKT Tanzania katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc utakaofanyika majira ya saa 10 jioni katika uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo wa kiporo cha pili kwa wekundu wa msimbazi katika ligi Kuu baada ya Ijumaa iliyopita kuanza kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mashujaa Fc katika uwanja wa Kmc Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Simba Sc inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama  60 itakuwa wageni wa JKT Tanzania katika mbio za kuwania ubingwa ikiifukuzia Yanga sc kileleni yenye alama 70 inayolisaka taji kwa msimu wa nne baada ya kulishikilia kwa misimu mitatu mfululizo tangu ilipowanyang’anya watani zao mwaka 2020-2021.

banner

Simba imepania kupata ushindi ili kupunguza pengo la pointi dhidi ya Yanga sc ambao wao wamecheza mechi 26 dhidi ya 23 za watani wao hao.

Mara ya mwisho zilipokutana timu hizo,Simba Sc ilishinda bao 1-0 lililotokana na penalti ya Charles Jean Ahoua na rekodi zinaonyesha kuwa katika mechi tisa za Ligi kuu zilipovaana tangu 2018/19, Simba sc  imeshinda mara nane huku JKT ikishinda mechi moja tu kwa bao 1-0 lililofungwa Februari 2020 na Adam Adam.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited