Connect with us

Makala

Simba sc Kucheza za Kimataifa

Klabu ya Simba sc itashiriki katika michezo kadhaa ya kirafiki ya kimataifa kwa ajili ya kujiandaa kikamilifu na ligi kuu pamoja na michuano ya klabu bingwa barani Afrika itakayoanza mapema mwezi ujao.

Simba sc imetoa ratiba fupi ya michezo mbalimbali ya kimataifa ambayo itashiriki katika kipindi hiki cha mapumziko ya ligi kuu nchini kupisha michuano ya kimataifa ya kufuzu mashindano mbalimbali ambapo baadhi ya nyota wa klabu hiyo wamejiunga na kambi za timu zao za Taifa.

Katika ratiba fupi iliyotolewa na klabu hiyo inaonyesha kwamba itakua na mchezo wa kwanza August 28 dhidi ya Asante Katoko utakaochezwa nchini Sudan huku siku tatu baadae itacheza na Al Hilal hukohuko Sudan kisha watarejea nchini kucheza na timu ya AS Arta Solar ya Djibout mchezo ambao utafanyika nchini Tanzania.

Lengo kubwa la michezo hiyo ni kuiandaa timu kushiriki michuano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala