Connect with us

Makala

Simba Day Augusti 8

Klabu ya Simba sc imetangaza kwamba tamasha la kufungua msimu mpya la klabu hiyo maarufu kama Simba Day litafanyika siku ya Augusti nane mwaka huu maarufu kama siku ya nane ambayo kiserikali huwa ni sikukuu ya wakulima nchini.

Kupitia mitandao yake ya kijamii klabu hiyo imethibitisha kufanyika kwa tamasha hilo kubwa na maarufu nchini ambapo klabi hiyo hulitumia kama kuanza kampeni kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu ambapo hutambulisha wachezaji wapya na wale wa zamani pamoja na benchi la ufundi ambalo kwa sasa linaongozwa na kocha Zoran Maki kutoka ulaya mashariki.

Msimu klabu hiyo inatarajiwa kuwatambulisha rasmi mbele ya mashabiki siku hiyo ambapo mastaa kama Augustine Okrah,Nassoro Kapama,Moses Phiri,Victor Ackpan na Habib Kyombo huku pia ikitarajiwa kukamilisha sajiri mpya zingine tatu ambazo zinafanyiwa kazi mpaka sasa.

Msimu Simba sc imeweka kambi ya maandalizi ya msimu nchini Misri ikijipanga kurejesha ufalme wake hapa nchini ambao msimu huu umechukuliwa na Yanga sc ambao wamefanikiwa kuchukua mataji yote muhimu na rasmi ya ndani na baada ya tamasha la Simba day klabu hiyo itakua na mchezo wa ufunguzi wa msimu mpya wa ligi ambapo itacheza na mahasimu wao Yanga sc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala