Simba Ashindwa Kufurukuta Kwa Tanzania Prisons

0

Simba Sc ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu bara ,leo Octoba 22,2020 wamekubali kipigo kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa ligi msimu huu wa 2020/2021 cha bao 1-0 kutoka kwa Tanzania Prisons.

Mchezo huo ulichezwa uwanja wa Nelson Mandela ambapo alama tatu muhimu zilikwenda kwa Tanzania Prisons.

Bao la pekee la Tanzania Prisons lilipachikwa na Samson Mbangula kipindi cha pili cha mchezo dakika ya 49 ambapo alitumia kichwa kupachika bao katika lango la Simba Sc.

Leave A Reply

Your email address will not be published.