Connect with us

Makala

Serikali,Michezo Na Corona

Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa amesema kuwa wanasitisha masuala yote yanayohusu mikusanyiko ya watu isiyo ya lazima ikiwa ni kujikinga na ugonjwa wa Corona.

“Tumesitisha michezo yote inayokusanya makundi ya watu kama vile Ligi Kuu ya Tanzania, Ligi Daraja la Pili, Ligi Daraja la Kwanza, lakini pia michezo ya shule za msingi (Umitashumta), michezo ya shule za Sekondari (Umiseta) pamoja na ile ya mashirika ya umma kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia leo”alisema Majaliwa

“Kwa hiyo Wizara ya Habari na Utamaduni na Michezo yenyewe itawaandikia mashirikisho yake yote ya michezo ili kuwaambia kwamba kwa kipindi cha mwezi mmoja hiki watatakiwa kusimamisha ratiba hizo katika michezo inayochezwa kipindi hiki ili kupambana na virusi vya Corona”

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala