Sarpong Afurahia Ushindani Wa Ligi

0

Mshambuliaji mpya wa Yanga Sc ,Michael Sarpong ameweka wazi kuvutiwa na ushindani uliopo ligi kuu ya Vodacom baada ya kushiriki mechi mbili msimu huu.

Sarpong aliyetua Yanga mwezi uliopita akitokea klabu ya Rayon Sports ya nchini Rwanda tayari amefungua akaunti yake bao 1msimu huu kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons ambao ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1.

Mghana huyo amesema baada ya kucheza mechi mbili msimu huu, amebaini timu zote zimejipanga na anatarajia ushindani utakuwa hivyo kwa kila mchezo kwani lengo lake ni kuhakikisha anaisaidia Yanga kufanya vizuri na kushika nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi.

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.