Samatta Apata Mbadala Aston Villa

0

Aston Villa imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji ,Ollie Watkins akitokea timu ya Brenford kwa kandarasi ya miaka miatano.

Watkins amesajiliwa Aston Villa kwa paundi milioni 28 ambayo inaweza kufikia hadi Paundi 33 kwani amepewa kipaumbele kikubwa cha kuja kuchukua nafasi ya ushambuliaji katika klabu hiyo.

Kutokana na dau kubwa lililofanywa na klabu hiyo kwaajili ya Watkins,mshambuliaji na nahodha kutoka timu ya taifa Tanzania ,Mbwana Samatta anatakiwa ajipange upya ili kupigania nafasi hiyo.

Watkins mwenye umri wa miaka 24 amefanikiwa kufunga jumla ya mabao 26 msimu uliopita wa 2019/2020 katika ligi ya mabingwa.

Leave A Reply

Your email address will not be published.