Samatta Aanza Na Sare Fenerbahce

0

Derby ya Uturuki imewakutanisha jana Galatasary na Fenerbahce ambayo anaichezea nahodha wa timu ya taifa Tanzania (Taifa Stars),Mbwana Samatta na mchuano kumalizika kwa sare ya kutofungana.

Samatta aliyejiunga Fenerbahce kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Aston Villa inayoshiriki ligi kuu England aliingia dakika ya 66 kuchukua nafasi ya Mame Thiam akiwa na jezi namba 10 mgongoni.

Licha ya kuupata mpira mara chache ameonekana akisumbua timu pinzani pale ambapo anaupata mpira na amefanikiwa kuokoa mpira wa adhabu kwa kichwa uliokuwa ukitaka kutua kwenye lango lao.

Leave A Reply

Your email address will not be published.