Connect with us

Makala

Prisons,Singida Big Stars Wafungiwa

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetoa adhabu ya kutosajili kwa kipindi cha dirisha moja kwa klabu za Singida Big Stars na Tanzania Prisons Fc baada ya vilabu hivyo kusajili Wachezaji wenye mikataba na klabu nyingine bila kufuata taratibu husika za usajili.

Klabu ya Singida Big  Stars iliyopanda daraja la ligi kuu msimu huu ilimsajili golikipa Metacha Mnata akitokea klabu ya Polisi Tanzania bila kufuata taratibu huku akiwa na mkataba ambao ulikua bado haujaisha na huku klabu ya Prisons Fc yenyewe ilimsajili golikipa Musa Mbise wa Coastal Union ambaye nae alikua na mkataba na klabu hiyo bila kufuata taratibu za kawaida za usajili.

Kutokana na adhabu hizo klabu hizo zitakosa kushiriki katika dirisha dogo la usajili linalotarajiwa kufunguliwa mwezi desemba mwaka huu ambapo klabu nyingine zitatumia muda huo kufanya maboresho ya vikosi vyao kutokana na usajili waliofanya katika dirisha kubwa la usajili.

Kamati imezikumbusha Klabu zote Nchini kuwa usajili wa Wachezaji unafanywa kwa kuzingatia Kanuni, na ambazo zitakiuka zitachukuliwa hatua kama hizi ili kukuza mpira wa nchini kwa haki,usawa na nidhamu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala