Connect with us

Makala

Ole Gunnar Hatihati Kufukuzwa United

Tetesi zinaeleza kuwa bosi wa Manchester United ,Ed Woodward hatasita kumfuta kazi kocha mkuu wa miamba hiyo ya Oldtrafford,Ole Gunnar Solskajaer kama Man United itaendelea kupata matokeo mabovu msimu huu.

Licha ya kuwa na ukumbusho wake mzuri wa tangu 1999 ambapo alifunga bao dakika za majeruhi na kuipa Manchester United ubingwa wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich katika fainali iliyofanyika uwanja wa Nou Camp,amesisitiza kuweka kando hayo yote kwa ajili ya maendeleo ya baadae ya klabu.

Kibarua cha sasa cha Ole Gunna kinaanza kuhusishwa na kocha wa zamani wa Tottenham Hotspurs ,Mauricio Pochettino aliyefutwa kazi miezi 11 iliyopita na nafasi yake kukabidhiwa kocha wa zamani wa Man United,Jose Mourinho.

Pochettino hajakubali kunoa kikosi chochote tangu kufutwa kazi Spurs na kama Ole Gunnar anazidi kuleta matokeo hasi,basi atafunguliwa milango ya kutokea Old Trafford na ikiwezekana kocha huyo wa zamani wa Spus atakalibishwa kwa mashetani hao wekundu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala