Connect with us

Makala

Ole Gunnar Apokea Mvua Ya Mabao 6-1

Manchester United imeshushiwa mvua ya mabao 6-0 na Tottenham Hotspurs katika mchezo wa jana wa ligi kuu England uliofanyika Old Trafford na kupoteza pointi tatu muhimu mbele kikosi hicho kinachonolewa na Jose Mourinho ambaye pia aliwahi kuifundisha United.

United walianza kupachika bao la kwanza kupitia nyota wao Bruno Fernandez dakika ya 2 kwa mkwaju wa penalti ambapo lilisawazishwa dakika ya 4 na Tanguy Ndombele wa Spurs.

Mvua ya mabao iliendelea dakika ya 7 na 37 kupitia kwa Song Heung-min na Harry Kane ambaye pia alitupia mawili dakika ya 30 na huku lile alilopachika dakika ya  79 lilikuwa ni kwa penalti, Serge Aurier alipachika moja dakika ya 51.

Kikosi cha Ole Gunna kilimaliza mchezo kikiwa pungufu baada ya Anthony Martial kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 28 jambo lililoongeza ugumu kwa Manchester United kupenya ngome ya Spurs.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala