Home Makala Nyoni Fiti Kuwavaa Kenya

Nyoni Fiti Kuwavaa Kenya

by Sports Leo
0 comments

Beki mkongwe wa Tanzania Erasto Edward Nyoni ambaye alikua na majeraha yaliyomfanya kukosa mchezo wa ufunguzi wa fainali za mataifa ya Afrika(Afcon) dhidi ya Senegali  imeripotiwa amepona majeraha hayo na tayari ameshaanza mazoezi kamili na kikosi cha timu ya taifa kilichopo nchini Misri.

Erasto aliumia katika mechi ya kujiandaa na michuano hiyo dhidi ya Zimbabwe iliyoisha kwa timu hiyo kutoka sare huku pia Tanzania ilimpoteza beki mwingine Aggrey Morris ambaye ametolewa katika kikosi baada kugundulika majeraha yake yatachukua muda mrefu kupona na nafasi yake kuzibwa na David Mwantika.

Tanzania imepoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Senegali baada ya kukubali kipigo cha mabao mawili kwa bila na kesho Alhamisi wataivaa kenya katika mchezo wa pili utakaopigwa saa tano usiku.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited