Connect with us

Makala

Ni Senegal Afcon 2021

Timu ya taifa ya Senegal imeibuka mabingwa wa michuano ya mataifa ya Afrika(Afcon 2021) baada ya kuifunga timu ya Taifa ya Misri kwa mabao 4-2 kwa changamotonya mikwaju ya penati baada ya kutoka suluhu katika dakika 90 za mchezo.

Awali dakika za mwanzoni mwa mchezo Sadio Mane alikwatuliwa eneo la hatari na mwamuzi kuamuru ipigwe penati ambayo ilichezwa na kipa wa Misri Gabaski na matokeo hayo yalidumu mpaka dakika 90 za mchezo huku mwamuzi akiongeza dakika 30 ambazo nazo zilimalizika bila bila.

Changamoto ya mikwaju ya penati ilianza kwa Senegal kufunga pigo la kwanza huku nao Misri wakishinda pigo la awali lakini walikosa pigo la pili na Senegal nao wakikosa pigo la tatu na baadae Misri pia walikosa pigo la nne na ndipo Sadio Mane alipopata nafasi ya kwenda kumaliza pigo la tano na kufanikiwa kufunga.

Sasa Senegal wanakua mabingwa wapya wa Afcon 2021 ambaye ilibidi ifanyike mwaka jana lakini ilisimama kutokana na changamoto ya ugonjwa wa Uviko 19 na sasa mwakani itafanyika nchini Ivory Coast huku Senegel wakiingia katika historia baada ya kutwaa ubingwa huo kwa mara ya kwanza.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala