Heshima imewekwa na klabu ya Yanga sc baada ya kufanikiwa kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Usm Algers katika mchezo wa fainali ya pili ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika licha ya kukosa ubingwa kutokana na sheria ya goli la ugenini.
Kutokana na matokeo hayo ya 1-0 yamefanya matokeo ya jumla kuwa 2-2 lakini Usm Algers wamebebwa na faida ya kushinda magoli mengi ugenini tofauti na Yanga sc huku Yanga sc wakifanikiwa kuonyesha kiwango kizuri katika mchezo huo wa ugenini mbele ya mashabiki zaidi ya elfu sitini waliohudhuria mchezo huo.
Bao pekee la Yanga sc lilifungwa kwa penati na Djuma Shabani dakika ya saba ya mchezo baada ya Kennedy Musonda kuangushwa katika eneo la hatari akiuwahi mpira mrefu wa Djuma Shabani kutoka upande wa kulia mwa uwanja.
Hata hivyo mashabiki wa Usm Algers hawakua waungana kwa kupiga mafataki mengi uwanjani huku pia vijana wanaorusha mpira uwanjani wakifanya makusudi kwa kurusha mipira mingi uwanjani ili kupoteza muda.
Yanga sc ilitawala eneo la kiungo chini ya Salum Abubakari na Mudathir Yahaya waliokua na viwango bora kabisa katika mchezo huo huku Usm Algers wakifanikiwa kumdhibiti Fiston Mayele ambaye hakupata nafasi ya kufunga.
Yanga sc imekua timu ya kwanza kutoka nchini Tanzania kurejea na medali ya mshindi wa pili ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika hali iliyosababisha Rais Samia Suluhu Hassan kuwaalika ikulu kwa ajili ya chakula cha jioni.