Home Makala Ndumbaro Aishuhudia Tp Mazembe

Ndumbaro Aishuhudia Tp Mazembe

by Sports Leo
0 comments

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameshuhudia mchezo kati ya TP Mazembe ya DRC Congo dhidi ya Esperance Sportive de Tunis ya nchini Tunisia ikiwa ni mchezo wa mashindano ya African Football League uliofanyika nchini katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mchezo huo ulioisha kwa Mazembe kushinda 1-0 umeshuhudiwa pia na Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Hamis Mwinjuma na Katibu Mkuu Bw. Gerson Msigwa ambapo pia viongozi mbalimbali wa soka nchini walikuwepo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Mchezo huo ulipaswa kufanyika nchini Congo Drc lakini kutokana na sababu mbalimbali Tp Mazembe iliomba kutumia uwanja wa Benjamin Mkapa kama uwanja wa nyumbani ambapo wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa baada ya kupata umati mkubwa wa mashabiki walioingia uwanjani hapo.

banner

African Super League ni michuano mipya inayofanyika barani Afrika kwa ngazi za klabu ikijumuisha jumla ya timu nane ambazo zilichaguliwa kutoka kila kanda ambapo mwakani michuano hiyo itajumuisha jumla ya timu 24.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited