Connect with us

Makala

NBC Yaongeza Mzigo Bingwa Ligi Kuu

Bodi ya ligi kuu nchini imesema kwamba bingwa wa ligi kuu atajipatia kiasi cha shilingi za Kitanzania milioni mia sita ambazo zitatoka kwa wadhamini wawili ambao ni Azam Tv na beni ya biashara ya NBC ambaye ndie mdhamini mkuu wa ligi hiyo.

Hayo yamesemwa hii leo na afisa mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Almas Kasongo wakati wa kutambulisha kombe jipya la ligi lililotolewa na benki hiyo ambalo litakabidhiwa kwa bingwa wa ligi kuu msimu huu.

Katika hafla hiyo ya kutambulisha kombe jipya pia benki hiyo ilisema kuwa itatoa zawadi ya kiasi hicho cha pesa kwa bingwa huyo nchini huku kwa ujumla ikitoa kiasi cha Tsh 1.8 bilioni ambazo zitakua kwa ajili ya zawadi ambapo bingwa atapata milioni 100 huku mshindi wa pili milioni 50 na timu yenye nidhamu itapa kiasi cha milioni 20 za kitanzania.

Pia bodi ilifafanua kwamba bingwa wa ligi kuu atapatiwa kombe hilo kwa sharti akale nalo mwezi mmoja kisha alirejeshe na akifanikiwa kuchukua mara tatu atakabidhiwa moja kwa moja.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala