Connect with us

Makala

Namungo Fc Yatua kwa Mgunda

Klabu ya Namungo Fc inasemekana iko mbioni kuachana na  kocha Mwinyi Zahera ambapo sasa imeamua kutua kwa kocha Juma Mgunda kuionoa klabu hiyo katika ligi kuu ya Nbc sambamba na michuano ya kombe la Shirikisho la Crdb.

Namungo Fc inafikiria kuachana na kocha Mwinyi Zahera baada ya kufungwa michezo miwili mfululizo katika ligi kuu ya Nbc katika uwanja wa nyumbani wa Majaliwa ikifungwa na Tabora United 2-1 na dhidi ya Fountain Gate Fc ikakubali kipigo cha mabao 2-0.

Kufuatia Vipigo hivyo,Mtendaji mkuu wa klabu hiyo Omary Kaya aliamua kujiuzuru nafasi yake hiyo huku mabosi wakijadiliana kuhusu hatma ya Zahera.

Mgunda anatajwa na mabosi wa klabu hiyo kutokana na uzoefu wake alipokua anaifundisha timu ya Coastal Union kisha akajiunga na Simba sc ambapo sasa amehamishiwa timu ya wanawake wa klabu hiyo (Simba Queens).

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala