Home Makala Nabi,Mgunda Mambo Fresh Caf

Nabi,Mgunda Mambo Fresh Caf

by Sports Leo
0 comments

Makocha wote wawili wa klabu za Simba sc na Yanga sc Nasredine Nabi na Juma Mgunda wamefanikiwa kukaa katika mabenchi ya ufundi ya klabu zao katika michezo wa klabu bingwa barani Afrika iliyomalizika hivi jioni ya leo.

Mgunda amefanikiwa kuiongoza Simba sc katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Nyassa Big Bullets ugenini mabao ya Moses Phiri na John Bocco huku Nabi alikuwepo benchi katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Zalan Fc mabao ya Fiston Mayele na Feisal Salum uliofanyika katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam.

Awali kulikua na sintofahamu kuhusu makocha kama wataziongoza timun hizo baada ya taarifa kuzagaa kuwa hawana vigezo vya kukaa benchi kutokana na kutomiliki leseni za juu za Caf za ukocha lakini kukaa kwao katika mabenchi ya ufundi kumetokana na Caf kuwaidhinisha baada ya kupitia wasifu wao na kuwaruhusu kukaa katika mabenchi ya ufundi ya klabu hizo kama makocha wakuu.

banner

Simba sc imemuajiri Juma Mgunda kama kocha wa mpito baada ya kuachana na kocha Zoran Maki ambaye amepata dili nono nchini Misri na kukubaliana na uongozi wa klabu ya Simba sc kuvunja mkataba.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited