Connect with us

Makala

Nabi Kupewa Heshima Maalum

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC ambao utapigwa jioni ya leo siku ya Jumatano katika uwanja wa Benjamin Mkapa, kutafanyika tukio maalum katika dakika ya 43 ya mchezo ili kumpa heshima kocha wao Nasreddine Nabi.
Tukio hilo ni kumpongeza Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi na benchi lake la ufundi kwa kuiongoza Yanga kucheza mechi 43 mfululizo za ligi pasipo kupoteza ambapo Itakapofika dakika ya 43, mashabiki watasimama na kupiga makofi kwa dakika moja ni ishara ya pongezi kwa benchi la ufundi kutokana na kuweka rekodi hiyo ya kibabe.
Nabi mpaka sasa hajapoteza mchezo wowote wa ligi kuu tangu apoteze kwa 1-0 dhidi ya Azam Fc katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika mwishoni mwa msimu 2020 kwa bao la shuti la mbali kutoka kwa mshambuliaji Prince Dube hali ambayo imewapa jeuri mashabiki wa klabu hiyo kutamba kwa sasa wakijivunia rekodi hiyo.
Hata hivyo Yanga sc inabidi wajipange wanapokwenda kuwavaa Kmc ambao kwa sasa wamekua na moto katika ligi huku wakizitoa jasho timu kubwa ambapo walitoa suluhu na Simba sc na kuwafunga Azam Fc kwa mabao 2-1 hali iliyosababisha kocha Dennis Lavigne kutimuliwa kikosini humo siku chache zilizopita.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala