Connect with us

Makala

Mvua Yasitisha Mechi Ya Kirafiki

Kutokana na mvua kubwa kunyesha leo Jijini Dar-es-salaam,imepelekea mechi ya kirafiki ya Simba Sc dhidi ya Ndanda Fc kughairishwa.

Mechi hiyo ilitakiwa kuchezwa leo Octoba 13, majira ya saa 11:00 jioni uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi kwa dhumuni la kuviweka sawa vikosi hivyo katika michuano yao ijayo na timu zingine.

Simba Sc ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu ,kwa sasa inashiriki ligi kuu bara msimu wa 2020/2021 huku Ndanda Fc iliyoshuka msimu uliopita wa 2018/2019 inashiriki ligi daraja la kwanza tayari kujiweka sawa kwa msimu ujao wa ligi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala