Munich Hawakamatiki Uefa Champions

0

Bayern Munich ambao ni mabingwa watetezi wa UEFA Champion League wamezidi kuwasha moto katika michuano msimu huu wa 2020/2021 baada ya kupata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Atletico Madrid kwenye mchezo wa jana Octoba 21.

Mabao ya Bayern Munich yalipachikwa na Kingsley Coman dakika ya 28 na 72,Leon Groetzka dakika ya 41 huku dakika ya 66 Corentin Tolisso alipachika bao lake.

Munich wanaendelea kuwa na wakati mzuri tangu ligi ya mabingwa kuanza huu ukiwa ni mchezo wao wa tisa chini ya kocha wao ,Hensi Flick wakiwa wameshinda mechi zote kwa kufunga jumla ya mabao 34 na wao kufungwa manne pekee

Leave A Reply

Your email address will not be published.