Tuendelee kusubiri kupoteza mchezo kwa klabu ya Yanga sc baada ya leo kufanikiwa kusawazisha dakika ya 76 ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Prisons mchezo mgumu uliochezwa ugenini katika uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga.
Jumanne Elifadhili aliipatia bao la uongozi Prisons akimalizia faulo kutoka upande wa kulia mwa lango la Yanga sc dakika ya 52 lakini Saido Ntibazonkiza alisawazisha dakika ya 76 na kufanya mchezo kumalizika kwa sare ya 1-1 huku akifunga bao la pili la ligi msimu huu.
Sasa Yanga sc imefikisha alama 44 ikicheza michezo 18 ya ligi kuu ikiwa katika nafasi ya kwanza ya msimamo huku Prisons wakisalia nafasi ya 9 na alama 22 za ligi kuu.