Connect with us

Makala

Morrison,Mayele Balaa Tupu

Ni balaa tupu kombinesheni ya wachezaji wa Yanga sc hasa Benard Morrison na Fiston Mayele ambao wameiwezesha klabu ya Yanga sc kuibuka na ushindi wa mabao mawili dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu nchini mzunguko wa pili uliofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta jijini Arusha.

Iliwachukua Yanga sc dakika tatu pekee kuandika bao la kwanza kupitia kwa Benard Morrison aliyemalizia pasi nzuri ya Jesus Moloko ambaye aliwahadaa mabeki kufuatia kupokea pasi safi ya Feisal Salum kutoka katikati ya uwanja.

Hertier Makambo ambaye alianza kama mshambuliaji wa kati alibanwa na mabeki wa Coastal Union kiasi ikamlazimu kocha Mohamed Nabi kumuingiza Fiston Mayele katika kipindi cha pili na kufanikiwa kufunga bao nzuri akimalizia pasi ya kichwa na Djuma Shabani aliyepata krosi ya kona kutoka kwa Benard Morrison dakika ya 61.

Yanga sasa imekaa katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi ikiwa na alama 6 na mabao manne huku Simba sc imekaa kileleni mwa msimamo kutokana na kuwa na alama 6 lakini ikiwa na wastani wa mabao matano ya kufunga na kufunga.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala