Home Makala Morisson Wa Simba Atajwa Yanga

Morisson Wa Simba Atajwa Yanga

by Sports Leo
0 comments

Yanga Sc imemtangaza Benard Morisson kuwa ni miongoni mwa wachezaji wake wakati wakiwatambulisha wachezaji wapya na wale waliokuwa kwenye kikosi hicho msimu wa 2019/2020 katika siku yao ya kilele cha wiki ya wananchi uwanja wa Mkapa,jijini Dar-es-salaam.

Wakati wa utambulisho wa wachezaji hao mtangazaji, Maulid Kitenge alisema kuwa mchezaji namba 28 ambaye ni banard Morrison bado ni mchezaji wa Yanga japo ameshatambulishwa na watani wao wa jadi Simba Sc na leo ni mechi yake ya kwanza dhidi ya Namungo Fc katika ngao ya jamii akiwa ndani ya Simba Sc.

Katika mabao 2-0 ya Simba Sc waliyopigwa Namungo Fc,Benard Morisson amehusika katika bao la pili ambapo lilidumu dakika 90 za mchezo na kuwapatia Simba Sc taji la ngao ya jamii

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited