Connect with us

Makala

Mlandege Fc Mabingwa Mapinduzi Cup 2023

Ni mshtuko mkubwa kwa mashabiki wa soka nchini Tanzania baada ya Mlandege Fc ya visiwani Zanzibar kufanikiwa kuwafunga Singida Big Stars 2-1 katika mchezo wa fainali ya kombe la Mapinduzi 2023 uliofanyika katika uwanja wa Amani visiwani humo.

Mashabiki wengi wa soka nchini walitarajia Singida Big Stars kuibuka na ushindi na kurudi na kombe hilo Tanzania bara lakini ndoto hizo zilianza kufifia mapema dakika ya saba ya mchezo baada ya Bashima Saite kufunga bao la kwanza kwa wenyeji licha ya kuwa na wachezaji wasio na majina makubwa kama wale wa wapinzani wao.

Mshangao mkubwa ulitokea kwa mara ya pili baada ya Mlandege Fc kupata bao la pili dakika ya 19 ya mchezo likifungwa na Abdulnasir Mohamed na mpaka mapumziko matokeo yalikua 2-0 lakini dakika sita tu baada ya kipindi cha pili Francy Kazadi alifunga bao la kwanza kwa Singida Big Stars kwa kichwa akimalizia mpira ulioshindwa kuokolewa na mabeki wa Mlandege Fc.

Kuingia kwa bao hilo kuliwaamsha Mlandege Fc walioingia na mfumo wa kuzuia pamoja huku wakishambulia kwa kasi na kuwapa wakati mgumu mastaa wa Singida Big Stars wakiongozwa na Bruno Gomes aliyedhibitiwa ipasavyo huku Deus Kaseke,Said Ndemla,Yussuph Kagoma,Ennock Atta Agyei wakiwa hawana la kufanya.

Baada ya dakika tisini za mwamuzi Mlandege Fc wamefanikiwa kuwa mabingwa wakibeba kombe hilo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 10 kupita huku mchezaji wa Singida Big Stars Yusuph Kagoma akichukua tuzo ya mchezaji bora wa michuano hiyo na Francy Kazadi akichukua tuzo ya mfungaji bora wa michuano huku Golikipa wa Mlandege Mpelure akichukua tuzo ya kipa bora na kinda bora akiwa ni Said Mussa wa Mlandege Fc.

Michuano hiyo ya kombe la Mapinduzi hufanyika kila mwaka mwezi Januari ikiwa ni moka ya shangwera kuelekea kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika 12/1/1964.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala