Connect with us

Makala

Mido la Kibabe Latua Simba sc

Klabu ya Simba sc imefanikiwa kumtambulisha mchezaji Ismaël Sawadogo mwenye umri wa miaka 26 baada ya kumsajili kwa mkataba wa miaka miwili akiwa kama mchezaji huru baada ya kumalizana na timu yake ya Difaa Hassan El-Jadid inayoshiriki ligi kuu nchini Morocco.

Sawadogo raia wa Burkina Faso anajiunga na Simba sc ikiwa ni usajili wa pili baada ya Saido Ntibanzokiza kwa lengo la kumaliza tatizo la uhaba wa viungo wakabaji kikosini humo ambapo timu hiyo imekua na nyakati ngumu hasa akikosekana Sadio Kanoute eneo la katikati.

Mchezaji huyo amezichezea klabu zifuatazo kwa mujibu wa mtandao wa Transfer Markets unajihusisha na historia na takwimu za wachezaji ambapo alianza na Rc Kadiogo,Al Mabarra Club ya nyumbani kwao Burkina Faso kisha Salitas Fc,US Ouagadougou,Al-Arabi SC ya ligi kuu nchini Kuwait,AS Douanes ya Burkina Faso na akaelekea Enppi SC ya Misri na akatua Diffaa ambapo alipotoka hapo akajiunga Simba sc.

Sawadogo anasifika kwa kuwa mwepesi wa kuzima mashambulizi ya wapinzani huku akitumia mguu wa kushoto ambapo pia anauwezo wa kucheza nafasi ya beki wa kati.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala